MASTAHIKI MEYA WA MANISPAA MJINI ZANZIBAR ZIARANI NCHINI UJERUMANI
MSTAHIKI Meya wa Baraza la Manaispa Mjini Zanzibar Ali Haji Haji, amefanya ziara maalum ya kikazi Nchini Ujerumani ambapo amepata fursa ya kutembelea moja ya nyumba maarufu Jijini Berlin na kupata kujua historia ya jengo hilo ambalo linadaiwa kujengwa mwaka 1390
Akizungumza Jijini Berlin Meya huyo alisema amejifunza vitu vingi kupitia jengo hilo ikiwa ni pamoja na kutunza maeneo ya kihistoria kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae.
Alisema Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla wanalo jukumu la kuheshimu na kuthamini vitu walivyokuwa navyo vya vivutio kwani vitu hivo ni hazina tosha kwa nchi na taifa kwa ujumla.
Aidhaa Ali aliwataka Wazanzibar kuwa na utamaduni wa kwenda maktaba kwa lengo la kukuza ujuzi na maarifa kwa manufaa yao.
Nae Afisa Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Jiji la Postdam nchini Ujerumani Ndg Issabel alisema jengo hilo ni muhimu kwa nchi ya Ujerumani kwani limechukua historia kubwa ya nchi hio na kuwa moja ya Makumbusho makubwa ya nchi hio.
Ziara hio bado inaendelea ambapo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mjini Zanzibar anatarajiwa kukutaa na kufanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa Jiji la Potsdam Mh Pete HeuerSeptemba16 mwaka huu majira ya saa saba za mchana sawa na saa sita za mchana kwa saa za Afrika Mashariki.
Ikumbukwe kuwa ziara hio ni kuimarisha uhusiano baina ya manispaa ya mji wa Zanzibar na Jiji la Potsdam uhusiano ambao uliasisiwa tangu mwaka 2011 na kuwekwa saini 2017.
MANISPAA MJINI IMEKUSANYA BILION MBILI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024
Na Muandishi Wetu.
BARAZA LA MANISPAA MJINI LIMEFANIKIWA KUKUSANYA ZAIDI YA SHILLINGI BILIONI MBILI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 SAWA NA ASILIMIA 80.
AKIWASILISHA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA BARAZA HILO KWA KIPINDI CHA ROBO YA PILI MKUU WA IDARA YA MAPATO,UCHUMI NA UJASIRIAMALI KUTOKA BARAZA HILO BI AMINA SIMAI MSARAKA AMESEMA MAKUSANYO HAYO YAMEONGEZEKA KUTOKANA NA KUWEPO KWA VIANZIO VIPYA VYA UKUSANYAJI WA MAPATO NDANI YA MANISPAA HIYO.
AMESEMA KUWA BARAZA HILO LITAENDELEA NA JUHUDI MBALIMBALI ZA KUIMARISHA MAPATO IKIWA PAMOJA NA KUTAFUTA MAENEO MAPYA YA WAWEKEZAJI ILI KUONGEZA WIGO WA UKUSANYAJI WA MAPATO NCHINI.
"KATIKA JITIHADA HIZO HIVI SASA TUNATAFUTA MSHAURI ELEKEZI KWA AJILI YA KUANDAA MAANDIKO YA MIRADI MBALIMBALI NA MIPANGO YA BIASHARA KWA MRADI WA FUNGUNI NA MIKUNGUNI",ALISEMA MKUU HUYO.
KUHUSU UTEKELEZAJI,MKUU HUYO ALISEMA BARAZA LINASIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO NA KUFANIKIWA KUFUNGA TAA 120 ZA MITAANI KATIKA WADI YA KIKWAJUNI,RAHALEO NA CHUMBUNI AMBAPO HADI SASA JUMLA YA TAA 60 LIMESHAKAMILIKA.
AIDHA ALISEMA HATA HIVYO WATAONGEZA USIMAMIZI NA UFUATILIAJI WA WATENDAJI KATIKA VITENGO VYA MAPATO IKIWEMO LESENI, MAEGESHO NA KUENDELEA KUFANYA OPERESHENI ZA LESENI ZA BIASHARA.
ALISEMA KUMEKUWA NA HUDUMA BORA KWA WAFANYABIASHARA KWA KUSAJILIWA NA KUPATIWA VITAMBULISHO WAFANYABIASHARA WADOGO AMBAPO KWA KIPINDI CHA OKTOBA HADI DISEMBA 2023 JUMLA YA WAFANYABIASHARA 65 WAMESAJILIWA KATI YA HAO 21 WAMELIPA NA TAYARI WAMESHAPATIWA VITAMBULISHO VYAO
MADIWANI WA BARAZA LA MANISPAA MJINI WAMELIOMBA BARAZA KUENDELEA KUTOA ELIMU JUU YA KULIPA ADA KWA HIARI KWA WAFANYA BIASHARA ILI KUONGEZA MAPATO
WASEMA BADO KUNA BAADHI YA WAFANYABIASHA HAWALIPI LESSENI KWA WAKATI NA KUSABABISHIA BARAZA HILO KUKOSA MAPATO YAKE IPASAVYO HALI AMBAYO INAREJESHA NYUMA JUHUDI ZA MAENDELEO HAPA NCHINI.
KIKAO HICHO KIMEFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MADIWANI KWA AJILI YA KUJADILISHI SHUGHULI ZA UTEKELEZAJI WA BARAZA LA MANISPAA MJINI KWA KIPINDI CHA ROBO YA PILI KW MWAKA 2023/2024.
MWISHO.
BARAZA LA MANISPAA MJINI LACHUKUA HATUA YA KUVUNJA MADUKA
BARAZA la Manispa Mjini limechukua hatua ya kuvunja maduka yaliojengwa katika maeneo ya wazi mtaa wa Nyerere Wilaya ya Mjini Unguja.
Akizungumaza baada ya kuvunjwa kwa maduka hayo Mkurugenzi wa Baraza la Manispa Mjini Ali Khamisi Mohammed alisema watu waache tabia ya kujichukulia hatua ya kujenga katika maeeneo ya wazi ili kuepuka rungu la kuvunjiwa nyumba au maduka yao.
Alisema Baraza la Manispaa Mjini halitamvumilia mtu yoyote atake chukua hatua ya kujenga katika maeneo ya wazi mbayo hayaja idhinishwa kwa ajili ya ujenzi na badala yake kuvunjiwa nyumba hiazo.
BARAZA LA MANISPAA MJINI LACHUKUA HATUA YA KUVUNJA MADUKA. . . .
BARAZA la Manispa Mjini limechukua hatua ya kuvunja maduka yaliojengwa katika maeneo ya wazi mtaa wa Nyerere Wilaya ya Mjini Unguja.
Akizungumaza baada ya kuvunjwa kwa maduka hayo Mkuruge . . . .
MASTAHIKI MEYA WA MANISPAA MJINI ZANZIBAR ZIARANI NCHINI UJE. . . .
MSTAHIKI Meya wa Baraza la Manaispa Mjini Zanzibar Ali Haji Haji, amefanya ziara maalum ya kikazi Nchini Ujerumani ambapo amepata fursa ya kutembelea moja ya nyumba maarufu Jijini Berlin na kupata . . . .
MANISPAA MJINI IMEKUSANYA BILION MBILI KWA MWAKA WA FEDHA 20. . . .
Na Muandishi Wetu.
BARAZA LA MANISPAA MJINI LIMEFANIKIWA KUKUSANYA ZAIDI YA SHILLINGI BILIONI MBILI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 SAWA NA ASILIMIA 8 . . . .
Huduma
Huduma zetu